Mkuu wa wilaya ya Malinyi wakili Sebastian Waryuba ameisifu Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri hiyo na kufanya kwa kipindi cha robo ya tatu ya kusanyaji kufika asilimia 99.5.
Mhe. Wakili Waryuba ameyasema hayo Aprili 24, 2025 katika Mkutano wa kawaida Baraza la Madiwani ulioketi kujadi taarifa za utekelezaji robo ya tatu 2024/ 205 ambapo Mhe. Waryuba alishauri Baraza hilo kuongeza kubuni vyanzo vipya vya mapato vitakavyosaidia kupata fedha ya kumalizia miradi mbalimbali iliyopo wilayani humo.
Naye Khamisi Katimba ni mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Malinyi amebainisha sababu zilizopelekea Halmashauri hiyo kufanikiwa ni pamoja na mshikamano Miongoni wa Waheshimiwa Madiwani,Watendaji pamoja na Watalam.
Aidha mkurugenzi Mtendaji Katimba ameongeza kuwa katika jitihada za kufikia hapo ni pamoja na kuhakikisha kuwa mianya yote inayosababisha utepotevu wa mapato inadhibitiwa.
Naye Khamisi Katimba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Malinyi amebainisha sababu zilizopelekea Halmashauri hiyo kufanikiwa ni pamoja na mshikamano Miongoni wa Waheshimiwa Madiwani,Watendaji pamoja na Watalam.
Aidha mkurugenzi Katimba ameongeza kuwa katika jitihada za kufikia hapo ni pamoja na kuhakikisha kuwa mianya yote nayosababisha utepotevu wa fedha inadhibitiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.