Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Malinyi Ndugu James Kikwesha ametoa taarifa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi imepokea Malipo ya Ruzuku ya Walengwa wa TASAF. Taarifa hiyo ameitoa tarehe 22 Agosti 2025.
Taarifa hiyo inaonesha Dirisha la Malipo la Mwezi Mei/Juni 2025 kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi imepokea Jumla ya Fedha Shillingi Millioni 96,564,000.00 kwa ajili ya Walengwa wa Mpango wa TASAF. Walengwa 1691 sawa na Asilimia Sabini (70%) ya Walengwa wote wamepokea Shillingi Millioni 64,873,500.00 kwa njia ya Mitandao ya Simu na Benki.
Walengwa 837 wamepokea Shillingi Millioni 31,690,500.00 kwa njia ya Fedha Taslimu, Hivyo Jumla ya Walengwa 2520 kutoka Vijiji 31 vya Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi wamepokea Shillingi Millioni 96,564,000.00 katika Dirisha la Malipo la Mwezi Mei /Juni 2025
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.