Mkuu wa wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba ameipongeza Timu ya Watumishi Sports Club kwa kushika nafasi ya kwanza katika mchezo wa kutupa vishale ( darts) kwa wanawake Kitaifa katika mashindano ya SHIMISEMITA 2024.
Mhe Waryuba ametoa pongezi hizo leo septemba 10, 2024 ofisini kwake wakati Timu hiyo ilipomtembelea ikiongozwa na Maimu Mkuu wa Kitengo cha Sanaa Michezo na Utamaduni Ndugu Omary Seif.
Mhe Waryuba amesema kuwa ushindi huo wa kishindo umeiheshimisha Wilaya ya Malinyi na hivyo amemtaka Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Sanaa, Michezo na Utamaduni kufanya jitihada za kuisajili timu hiyo ilikuwa rahisi kupata wadau mbalimbali watakao unga mkono juhudi za Halmashauri katika sekta ya michezo
Nae kaimu mkuu wa kitengo cha sanaa michezo na utamaduni ndugu Omary Seif ameishukuru ofisi ya mkuu wa Wilaya, ofisi ya Mkurugenzi kwa kuiwezesha timu hiyo kushiriki katika mashindano ya SHIMISEMITA 2024 jijini Mwanza
Katika mashindano hayo ya SHIMISEMITA 2024 Timu ya Watumishi Sports Club imeshiriki katika michezo ya ndani ikiwa ni pamoja na mchezo wa bao, mchezo wa kurusha vishale (darts), mchezo wa draft na karata
Katika mchezo wa darts kwa upande wa wanawake Timu ya Watumishi Sports Club imeshika nafasi ya kwanza, mchezo wa bao kwa wanaume imeshika nafasi ya tatu, mchezo wa draft kwa wanaume imeshika nafasi ya kumi na sita, mchezo wa karata kwa wanaume imeshika nafasi ya kumi na sita, na mchezo wa karata kwa wanawake imeingia katika hatua ya makundi
Kufuatia hali hiyo tTimu ya Watumishi Sports Cub imepata zawadi ya kombe la mshiriki wa kwanza kwa mchezo wa dats na kombe la mshindi wa tatu kwa mchezo wa bao pamoja na cheti cha ushiriki.
Mashindano hayo ya michezo ya Watumishi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa Tanzania ( SHIMISEMITA) yalianza Agosti 25, 2024 na kumalizika septemba 6, 2024 jijini Mwanza.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.