Hayo yamesemwa leo Machi 20, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Vijiij, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji juu ya utekelezaji wa majukumu yao katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mhe. Waryuba amesema kuwa ni wajibu wa Viongozi hao katika ngazi za Vijiji na Vitongoji kuitisha mikutano ya vijiji pamoja na kujibu hoja za Wananchi juu ya mwenendo wa Serikali ya Kijiji husika.
Aidha, Mhe. Waryuba ameielekeza Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kuhakikisha kuwa Watendaji wa Vijiji wa kujitolea wanawezeshwa kielimu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa usahihi na kuhakikisha kuwa wana mikataba inayowaunganisha na Halmashauri kama dhamana ya kazi zao katika Kijiji husika.
Mafunzo haya ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji yamefanyika katika Tarafa ya Malinyi, Ngoheranga pamoja na Mtimbira..
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.