Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Wilayani Malinyi Mkoani Morogoro leo Septemba 15, 2024 imehitimisha ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Tarafa ya Mtimbira ambapo jumla ya ya miradi 6 ya maendeleo imekaguliwa katika Tarafa hiyo.
Miradi hiyo 6 iliyokaguliwa ni pamoja na Mradi wa umeme Itete Minazini, Mradi wa jengo la Mama na Mtoto katika Kituo cha Afya Itete, Mradi wa Barabara Ipera Asilia, Ujenzi wa tenki la maji mnadani Njiwa, Ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum shule ya msingi Mtimbira, pamoja na Mradi wa ujenzi wa zahanati ya Usangule.
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi ilianza ziara hiyo ya ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya CCM Septemba 13, 2024 katika Tarafa ya Malinyi ambapo jumla ya miradi 6 ilikaguliwa, Tarafa ya Ngoheranga miradi 5 ilikaguliwa na hivyo mpaka mwisho wa ziara hiyo jumla ya miradi 17 ya maendeleo imekaguliwa na kutolewa maelekezo.( Elimu, Afya, Maji, Umeme na Miundombinu ya barabara )
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.