Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba leo Disemba 6, 2024 amewaongoza Wakazi, Wafanyabiashara wa eneo la njia panda katika Kijiji cha Misegese Wilayani Malinyi pamoja na Watumishi wa Halmashauri kufanya usafi wa mazingira katika soko la njiapanda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 9 Disemba.
Mhe. Waryuba ametoa rai kwa Wakazi wa Malinyi kulifanta zoezi la usafi wa mazingira kuwa endelevu ili kulinda mazingira ya soko hilo pamoja na afya za Wafanyabiashara wa eneo hilo.
"Suala la usafi ni pamoja na usafirishaji wa taka kwenda sehemu sahihi ikiwa ni pamoja na nyinyi Wafanyabiashara kuwa na vizimba vidogovidogo pamoja na mashimo ya takataka ambayo wakati mwingine siyo lazima kutumia njia hii mnayoitumia hivi sasa" amesema Mhe. Waryuba.
Akizungumzia ujenzi wa vibanda vilivyopo katika soko hilo Mhe. Waryuba amesema ujenzi wa vibanda hivyo haukufuata utaratibu unaotakiwa hivyo amemuelekeza kiongozi wa Wafanyabiashara wa eneo la njia panda kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwaajili ya kupata maelejezo zaidi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.