Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amesema kuwa Wilaya ya Malinyi inategemea sana uchumi wa biashara yaani kilimo biashara, mifugo biashara,uvuvi biashara na ushirika biashaara, hivyo Serikali itahakikisha kuwa kila uchumi unaofanyika Malinyi unakuwa ni uchumi wa kibiashara lengo likiwa ni kuhakikisha uchumi unaendela kukua , mzunguko wa fedha unaongezeka ili Halmashauri ipate mapato, Serikali ipate kodi na Wananchi wapate kipato cha kuendeleza maisha.
Mhe. Waryuba ameyasema hayo Disemba 10, 2024 wakati akifunga kikako cha Baraza la Biashara la Wilaya kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
Sambamba na hilo Mhe. Waryuba amewasihi Wadau wa Biashara kutumia Taasisi za fedha kwaajili ya kupata mikopo ambapo maetoa rai kwa Taasisi hizo kuweka mazingira wezeshi ili Wananchi waweze kupata mikopo hiyo kwa urahisi.
“Niwaombe sana sisi ambao tumebeba dhamana ya masuala mbalimbali kwa niaba ya Umma tuhakikishe kuwa Sekta binafsi wanakua ni wadau wetu na ni marafiki zetu, tutengeneze mustakabali huo kwasababu Sekta binafsi wakikaa vizuri na Serikali inakaa vizuri ili mahusiano ya biashara na kiuchumi yaendelee vizuri ndani ya Wilaya ya Malinyi” amesema Mhe. Waryuba
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Biashara Ndugu Msabaha Alawi amesema kuwa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri imeandaa program maalum itakayowashirikisha Wadau wa Biashara kuwajibika kulipa tozo stahiki kwa maendeleo ya Serikali ‘MALIZA MWAKA KIJANJA KWA KULIPA TOZO STAHIKI KWA MAENDELEO YA SERKALI’
Akifafanua kuhusu program hiyo Ndugu Alawi amesema kuwa kuanzia tarehe 11 , Disemba 2024 timu ya Wataalamu itapita maeneo yote ya kibiashara kwa lengo la kutoa elimu ya mifumo ya ulipaji wa tozo stahiki yaani ushuru, ada za leseni za biashara, usajili wa biashara, utoaji wa namba za malipo na utoaji wa leseni hapo kwa hapo, program hiyo inatarajiwa kumalizika tarehe 3/1/2025.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao cha Baraza la Biashara Wadau wa Biashara Wilayani Malinyi wamesema kuwa uchumi wa Malinyi unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja ubovu wa miundombinu ya barabara, na uchache wa vyanzo vya uchumi ambavyo ni kilimo na ufugaji kitu ambacho kinafanya biashara kuwa za msimu na inasababisha uchumi wa Malinyi kutokua imara, kufuatia hali hiyo Wadau hao wameishauri Ofisi ya Mkurugenzi kupitia Divisheni ya Biashara kubuni vyanzo vipya vya kukuza uchumi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.