Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba ametembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwenye Maonesho ya Nane Nane Kanda ya Mashariki 2025 yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere vilivyopo Manispaa ya Morogoro tarehe 1 Agosti 2025. Mkuu wa Wilaya aliambata na Katibu Tawala Ndugu Saida Abbass Mhanga.
Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kuangalia vipando mbalimbali vya Mazao vilivyopandwa pembezoni mwa Banda la Malinyi, pia ametoa maelekezo kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Wilaya Ndugu Absolum Gipson ambaye ni Mkuu wa Idara ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi ili kuboresha muonekano wa Banda la Maonesho.
Kauli Mbiu ya Nane Nane "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi,2025"
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.