Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amefanya Kikao juu ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani katika Wilaya ya Malinyi. Kikao hiko kimefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri tarehe 09Julai 2025.Kikao hiko kilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji, Wadau wa Vyama vya Ushirika na Wakulima wanufaika wa Stakabadhi Ghalani.
Nia ya Kikao hiko ilikuwa ni kujenga mustakabali wa Ushirika na kutoa changamoto za Stakabadhi Ghalani na Suluhisho lake.Mheshimiwa DC alisema amepata malalamiko mengi kuhusu Ushirika na Stakabadhi Ghalani hivyo alitoa maagizo kwa Mrajisi na Watu wa Ushirika wasaidie kutoa Elimu ya Ushirika kwa Wananchi. Kuwe na Checks and Balance kati ya Wakulima, Mtunza Ghala na Chama cha Ushirika.Ameagiza Wakulima walipwe kwa wakati, Kila Mkulima atumie Akaunti yake binafsi ya Benki.Orodha ya Wakulima wanaostahili kulipwa iende UKIKU haraka. Wasimamizi wa Ghala waweke Bima dhidi ya Uharibifu kama Moto,Wizi na Uharibifu wowote, Wakuu wa Idara wa Halmashauri wawaelimishe Wakulima jinsi ya kujaza Fomu.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.