Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mheshimiwa Sebastian Waryuba amewaongoza Wananchi wa Tarafa ya Mtimbira kwenye Bonanza la Kuhamasisha Shughuli za Maendeleo ambalo limefanyika kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Madibira Juu tarehe 13 Septemba 2025.
Bonanza hilo limehusisha Michezo mbalimbali ikiwemo Kukimbiza Kuku, Mashindano ya Kula, Kuvuta Kamba,Ngoma, Sarakasi na Mchezo wa Mpira wa Miguu kati ya Mtimbira vs Usangule, ambapo Usangule waliibuka na Ushindi wa Goli 1=0 na kukabidhiwa kombe la Ushindi.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi katika Hotuba yake alitoa Shukrani kwa Mheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa maboresho aliyoyafanya Malinyi katika kipindi chake cha Uongozi kwenye Sekta mbalimbali kama Elimu, Afya nk.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi amewaomba Wananchi waondoe Migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji na amewataka Wafugaji waende kuchanja Mifugo yao. Mheshimiwa Waryuba amewaomba Wananchi wawe Mabalozi wa Maendeleo ndani ya Kaya, Kijiji mpaka Kitongoji kila mmoja awe Balozi wa Maendeleo.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi amewaomba Wananchi kudumisha Amani na Usalama, amewataka Wananchi wapendane bila ya kubaguana. Mwisho amewaomba Wananchi Wajitokeze kupiga Kura ya Rais,Wabunge na Madiwani ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.