Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha suala la utolewaji wa chakula shuleni ni la lazima na endelevu.
DC Waryuba ameyasena hayo mapema Mei 15, 2025 katika kikao cha tathimini ya mkataba wa lishe robo ya 3 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ulipo katika Kijiji cha Misegese.
DC Waryuba pia amewataka Wataalam wa afya kuendekea kutoa elimu kwa Wananchi hususan akina mama Wajawazito juu ya madhara yatokanayo na kutokutumia kwa usahihi vidonge vya madini chuma na folic acid.
kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Daktari Julius Nyasongo amesema jamii ina mtazamo hasi juu ya vidonge vya madini chuma na folik acid kwa Wajawazito na hivyo wengi wao hawazitumii kwa usahihi na hivyo kupelekea madhara makubwa ikiwa ni pamoja na upungufu wa damu pamoja na magonjwa yatokanayo na uzazi.
katika kuhakikisha kuwa Wanafunzi wanapata chakula cha mchana wakiwa shule Matendaji wa Kata ya Mtimbira Ndugu Samweli Milangasi anasema moja ya changamoto anazokutana nazo kwenye Kata yake pale anapolazimika kuwakamata na kuwaweka ndani Wazazi wasochangia chakula cha Watoto shuleni ni Wazzi hao kutokua na uwezo wa kulipa gharama zinazotakiwa katika zoezi hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Viongozi wa dini Wilaya ya Malinyi, Shekhe wa Wilaya Ndugu Mohamed Nwinyi ameiomba Idara ya afya kuaandaa vipeperushi ambavyo vinaelimisha kuhusu umuhimu wa lishe ambavyo vitawasaidia Viongozi na Waumini wa dini zote kupata uelewa kuhusu umuhimu wa lishe.
Hata hivyo, Akizungmzia umuhimu wa lishe kwa vijana balehe Afisa lishe wa Wilaya Bi Bi Betrida Makuvila amesema vijana wengi wana upungufu wa damu unaosababishwa na ulaji wa vyakula visivyo na virutubisho.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.