Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Malinyi Ndugu Ahobokile Mwambwanje Songela amefunga rasmi mafunzo ya Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya Kata Jimbo la Malinyi. Mafunzo hayo yalianza tarehe 4 Agosti 2025 mpaka tarehe 6 Agosti 2025. Mafunzo hayo yaliyofungwa yalikuwa yanafanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi.
Ndugu Songela amewasisitiza Washiriki kuzingatia Mafunzo waliyopewa kwa mada zote 11 walizofundishwa na waviishi viapo vyao walivyoapa, Pia wafuate Katiba,Sheria,Kanuni,Miongozo na Maelekezo ya Tume Huru ya Uchaguzi na Wasome na Wazielewe Sheria ya Uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Namba 1 ya Mwaka 2024 na Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi Namba 2 ya Mwaka 2024.
Mafunzo hayo ya Siku Tatu yaliyokamilika ni sehemu ya kuwajengea uwezo watendaji hao kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.