Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Malinyi Ndugu Ahobokile Mwambwanje Songela amefungua Mafunzo kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata Jimbo la Malinyi yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Malinyi.
Ndugu Songela amesisitiza Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata katika Jimbo la Malinyi kuzingatia Sheria za Uchaguzi kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi chote cha Uchaguzi.
Kabla ya Ufunguzi wa Mafunzo hayo , Wasimamizi wa Uchaguzi 20 kutoka kata 10 za Halmashauri ya Malinyi walikula Kiapo cha kujitoa Uanachama wa Chama chochote cha Siasa na kiapo cha kutunza Siri. Kiapo hicho walikula mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Malinyi Ndugu James Clement Mwakalosi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.