Afisa Mwandamizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Ndugu Edna Stephen Assey ametoa Mafunzo kuhusu Maadili kwa Vyama vya Siasa na Vitendo vinavyokatazwa na Sheria ya Gharama za Uchaguzi wakati wa Uchaguzi. Mafunzo hayo yametolewa kwenye Ofisi za Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Malinyi zilizopo katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi tarehe 2 Agosti 2025.
Mada Mbalimbali zilijadiliwa kwenye Mafunzo hayo kama ifuatavyo;
Sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Haki na Wajibu wa Chama cha Siasa katika Uchaguzi, Vitendo vinavyokatazwa kwa Mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Adhabu Chini ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Marejesho ya Gharama za Uchaguzi na Wajibu wa Mtu kutoa taarifa kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kumlinda mtoa taarifa.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.