Hayo yamesemwa mapema Aprili 24, 2025 na Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega wakati alipofanya ziara ya kukagua athari za mvua za masika zinazoendekea kunyesha Wilayani Malinyi na kusabab8sha uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja
Mhe. Ulega amesema kuwa fedha hizo zitatumika kujenga daraja la Mto furua lililopo barabara ya Misegese Malinyi na daraja la Iragua lilopo kijiji cha Stendi ya Nyanya.
Pamoja na hayo, Waziri Ulega ameeleza kuwa Serikali pia imeridhia kutengeniza barabara ya Lupiro - Malinyi kwa kiwango cha lami ambapo barabara hiyo ina urefu wa zaidi ya km 100.
Awali akimkaribisha Mhe. Waziri kwaajili ya kuongea na Wananchi , Mkuu wa mkoa wa Morogoro Alhaji Adam Malima Alisisitiza zaidi kupatikana kwa suluhisho la kudumu katika maeneo hayo ili kuwaondolelea Wananchi wa maeneo Malinyi adha hiyo ambayo imekua ikijirudiarudia.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.