Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Malinyi Bi Rehema Rajabu amesema kuwa mikakati ya kudhibiti magonjwa ya mlipuko( kuhara na kutapika) iliyopangwa na Sekta ya afya Wilayani Malinyi iwashirikishe Watendaji walio karibu na Wananchi ili kujenga uelewa wa pamoja ambao utasadia katika kuinusuru Wilaya ya Malinyi kutokana na magonjwa hayo ya mlipuko.
Bi Rehema Rajabu ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha dharura cha Tathimini ya magonjwa ya mlipuko Wilaya ya Malinyi kilichofanyika Septemba 19, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Wadau mbalimbali wa sekta ya afya katika ngazi ya Wilaya.
Naye Kaimu Mjurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Bi Pendo Masalu amewataka Watendaji katika Kada zote kuchukua tahadhari na kushirikiana kwa pamoja katika kutokomeza magonjwa ya mlipuko Malinyi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi amemuelekeza Mganga Mkuu wa Wilaya kuitumia vyema Kamati ya kuzuia magonjwa ya mlipuko ngazi ya Wilaya katika kuratibu zoezi hili.
Mapema, akizungumza katika kikao hiko Mganga Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Dokta Julias Nyasongo amesema kuwa tayari timu za Wataalam wa afya zimepita katika maeneo mbalimbali Wilayani Malinyi na kutoa elimu kwa Wakazi wa maeneo hayo juu ya namna bora ya kujikinga na mlipuko wa magonjwa hayo.
Hata hivyo, Dokta Nyasongo ametoa wito kwa Wakazi wote wa Malinyi kuzingatia kanunu za afya ambazo zimeelekezwa na Wataalam wa afya ambao wamepita katika makazi yao ili kuepukana na magonjwa hayo ya mlipuko.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.