Mkuu wa wilaya ya Malinyi Mhe Sebastian Waryuba amesema kuwa ni muhimu kuwa na uhusiano mzuri kati ya Serikali Kuu na Serkali za Mitaa na kuongeza kuwa hakuna haja ya kutokuelewana kwani wote wanajenga nyumba moja.
Mhe. Waryuba ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya utawala bora yaliyofanyika leo Septemba 9, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuwahusisha Viongozi wa Chama, Wahe. Madiwani, Kamati ya Ulinzi na usalama, Wakuu wa Idara na Vitengo, Makatibu Tarafa, na Watendaji wa Kata
"Mafunzo haya elimishi, Mafunzo elekezi hayabagui, yamelenga kuelimisha , nawaomba Washiriki wote muyazingatie kwa umakini na mkayatumie katika utendaji kazi wenu na hasa katika kipindi hiki ambacho tupo katika maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuhakikisha zoezi hili la uchaguzi linaenda vizuri.
Aidha, Mhe, Waryuba amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Khamis Jaaphary Katimba kwa ubunifu wa kuandaa mafunzo hayo na kuongeza kuwa hayo ndio mambo muhimu aliyokua akitaka kuyaona yakifanyika katika Wilaya ya Malinyi.
Sambamba na Hilo, Mhe. Waryuba pia amewaomba Watumishi na Washiriki wa mafunzo hayo kumpa ushirikiano Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Wialaya ya Malinyi ili aweze kutekeleza najukumu yake kwa ufanisi
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambaye pia ni Diwani wa Kata ya mtimbira Mhe. Jane Komba amemshukuru Mhe. Waryuba kwa ufunguzi wa mafunzo hayo na kuongeza kuwa mafunzo hayo yataleta mabadiliko chanya katika utendaji kazi wa Washiriki katika kuwahudumia Wananchi katika maeneo yao.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi yalilenga kutoa elimu katika eneo la Utawala bora, Mipango na bajeti (Mahusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, Kanuni za kudumu za Halmashauri, uendeshaji wa vikao, vikao vya Kata na Vijiji, bajeti idhinishwa, Mapato ya ndani, Hoja za ukagauzi pamoja na taratibu za manunuzi.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.