Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba amewataka Wafugaji Wilayani humo kutowaachia Watoto jukumu ya kuchunga mifugo hali inayopelekea mifugo kuingia katika mashamba ya Wakulima na kusababisha uharibifu wa mazao pamoja na migogoro kati ya Wafugaji na Wakulima.
Mhe. Waryuba ameyasema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na Jamii ya Wafugaji Wilayani Malinyi katika mkutano wa Jamii hiyo ya Wafugaji uliofanyika katika Kijiji cha Misegese
Aidha Mhe. Waryuba amesema kuwa anakusudia kuunda umoja wa Wakulima katika ngazi zote za kata na kutakuwa na vikao kati ya Wakulima na Wafugaji ili kuleta ushirikiano baina yao.
Sambamba na hilo, Mhe Waryuba ametoa pongezi kwa wafugaji kutokana na umoja na ushirikiano walionao na kuwaomba waendelee na ushirikiano huo.
Nae Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ndugu Absalom Gepson amewataka Wakulima wanaotoa maeneo yao kwa ajili ya Wafugaji kuchungia mifugo yao wayatoe kwa maandishi na kuonesha mwisho wa mipaka ili kuondokana na migogoro ya wafugaji kulisha mifugo kwenye maeneo ya Wakulima.
Hata hivyo, Jamii ya Wafugaji Wilayani Malinyi pamoja na kuwaslisha taarifa ya mapato yatokanayo na mifugo waliweza pia kuwasilisha ombi kwa Mhe. Waryuba mkuhusu kupatiwa eneo kwaajili ya kunyweshea mifugo yao.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.