Hayo yamesemwa na Masimamizi wa uchaguzi Jimbo la Malinyi Ndugu Khamis Jaaphar Katimba Novemba 12, 2024 katika kikao cha 6 kilichofanyika katika Ofisi za Halmashauri baina yake na Viongozi wa vyama vya Siasa Wilayani Malinyi.
Ndugu Katimba amesema kuwa tangu kuanza kwa zoezi la uandikishaji amekuwa na utaratibu wa kukutana na Viongozi wa vyama vya siasa ili kufanya tathimini ya pamoja kwa yale yaliyopita, kupanga mikakakati ya masuala yanayotarajiwa kufanyika pamoja na kupeana elimu juu ya masuala ya uchaguzi na kuongeza kuwa mwendelezo wa vikao hivi vimesaidia kudumisha hali ya utulivu na Amani.
”Kwa maudhui ya leo tulikua tunajadili shughuli zilizo mbele yetu ikiwa ni pamoja na utayarishaji wa ratiba za kampeni, ufanyikaji wa kampeni, upigaji wa kura, kuhesabu kura pamoja na matokeo ya upigaji kura, tumekubaliana kuwa hiki ndicho kikao chetu cha mwisho kabla ya uchaguzi, na tunatarajia kukutana tena baada ya uchaguzi kama hakutakua na dharura itakayojitokeza hapa katikati kufanya tathimini ya zoezi zima la uchaguzi ”amesema Katimba
“Kutokana na misingi ambayo tumejiwekea inanipa matumaini mimi kama msimizi wa uchaguzi kuwa tutamaliza zoezi hili la uchaguzi vizuri, kwa Amani na upendo” amesema Katimba
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF wilaya ya Malinyi ndugu MIraji Ngapulila amesema vyama vya siasa vimeshirikishwa tangu mwanzoni mwa zoezi la uandikishaji na kwamba wameshiriki kikamilifu katika vikao 6 vilivyoitishwa na Msimamizi wa uchaguzi na wamejadili masuala mbalimbali yanayohusu uchaguzi.
“Kwaniaba ya vyama vya Siasa Wilaya ya Malinyi tunamshukuru Msimamizi wa Uchaguzi kwa ushirikiano aliotupatia tangu mwanzo wa zoezi hili,tunaomba ushirikiano huu uendelee hata baada ya uchaguzi, tuendelee kushirikishwa kwenye mambo mbalimbali ya kuiletea maendeleo Malinyi”amesema Ngapulila
Mwenyekiti huyo wa CUF Mlinyi amewaomba Wananchi wote Wa Malinyi waliojiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura wajitokeze kwa wingi tarehe 27/11/2024 waweze kuchagua Viongozi watakaowaongoza katika kipindi kingine cha miaka mitano.
Hata hivyo Ndugu Ngapulila amesema kuwa Viongozi wa vyama vya siasa Wilaya ya Malinyi wako tayari kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika na kumalizika kwa Amani na utulivu.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.