Waendeshaji wa vifaa vya Bayomtrik (BVR) na waandikishaji wasaidizi wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura wametakiwa kuifanya kazi hiyo kwa umakini wa hali ya juu
Hayo yamesemwa na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Malinyi Ndugu Khamis Jaaphar Katimba wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waendesha vifaa Bayometrik (BVR)na Waandikishaji wasaidizi wa uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga kura Jimbo la Malinyi yaliyofanyika februari 26 -27/2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Ndugu Katimba amewataka washiriki wa nafasi ya uendeshaji vifaa Bayometrik (BVR)na Waandikishaji wasaidizi kusimama kwa ufasaha katika nafasi zao na kwamba hatakuwa tayari kuona uzembe wa hali yoyote unajitokeza katika zoezi hilo.
Naye Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Malinyi Bi Sikujua Kimweri amewaasa Washiriki hao kufanya kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni, miongozo ya mafunzo na sheria za utumishi wa Umma ili kuepuka kuingia kwenye hatia na kuliingiza Taifa katika hasara.
Hata hivyo, Wawezeshaji wa mafunzo hayo kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa nyakati tofauti wamewataka Washiriki wa mafunzo hayo kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia miongozo ya mafunzo waliyoyapata ili zoezi hilo liweze kufanyika kwa weledi.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga kura kwa jimbo la Malinyi na Mkoa wa Morogoro linatarajiwa kuanza rasmi Machi 1/2025 na litakamilika Machi 7/2025.
‘KUJIANDIKISHA KUWA MPIGA KURA, NI MSINGI WA UCHAGUZI BORA’
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.