Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba Novemba 18, 2024 wakati akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mkindigili ya kukabidhi hundi ya mfano yenye thamani ya Zaidi ya shilingi 5000,000,000 kwa vikundi vinavyonufaika na mikopo ya 10% ya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu
Mhe. Waryuba amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu utolewaji wa mikopo hiyo yenye lengo la kuwakwamua Wananchi kiuchumi ili kuondokana na hali ya umasikini na amewataka Wanaufaika hao kuirejesha mikopo hiyo kwa wakati ili waendelee kuwa na sifa ya kukopesheka na kutoa nafasi ya vikundi vingingine viweze kukopa katika awamu zinazofuata.
Taarifa ya utekelezaji wa mchakato wa utoaji wa mikopo hiyo iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Ndugu Ahobokile Songela imeeleza kuwa tangu mwanzo mwa zoezi hilo Halmashauri ilipokea maombi ya mikopo kutoka kwa vikundi 228 Wilayani Malinyi lakini Kamati za uhakiki wa mikopo hiyo zilifanya uchambuzi na kupata vikundi 59 ambavyo ndivyo vyenye sifa ya kupata mikopo hiyo katika awamu hii ya kwanza.
Ndugu Songela amesema kuwa katika vikundi hivyo 59, vikundi 29 ni vya Wanawake, vikundi 24 ni vya Vijana na vikundi 6 ni vya Watu wenye ulemavu na hivyo kufanya idadi ya wanavukundi kufikia 410
Akizungumza kwa niaba ya Vijana wanaonufaika na mikopo hiyo Ndugu Vicent Lukumbo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji wa mikopo hiyo, Mhe. Sebastian Waryuba kwa usimamizi wa zoezi hilo la utoaji wa mikopo, na Ofisi ya Mkurugezi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi kwa kuendesha mchakato huo wa utoaji wa mikopo tangu mwazo mpaka zoezi hili lilipokamilika.
Naye Beatha Usanga muwakilishi wa vikundi vya Wanawake amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na amesema kuwa Wanawake wa Malinyi wapo pamoja na Mhe. Samia Suluhu Hassan katika nyakati zote.
Kwa upande wake Bi Marry Malangu muwakilishi wa Watu wenye ulemavu amawataka Watu wenye ulemavu wanaonufaika na mikopo hiyo kufanya kazi kwa bidii kwani Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hana mchezo katika kuhakikisha Wananchi wake wanajikwamua kiuchumi na kuondokana na hali ya umasikini.
Vikundi hivyo 59 vinajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo uendeshaji wa viwanda vidogovidogo, kilimo, ufugaji, usafirishaji pamoja na uwakala wa fedha.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.