Oktoba 5, 2024 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Ndugu Fadhili Rajabu Maganya amefanya ziara ya siku moja Wilayani Malinyi ambapo ametembelea mradi wa kituo cha afya Itete mradi wa maji Itete na baadae kukamilisha ziara yake kwa kuzungumza na Wanachama wa CCM katika Ofisi ya Chama tawi la Mtimbira.
Akiwa katika Kituo cha afya Itete Ndugu Fadhili Maganya ameelekeza Uongozi wa kituo hiko kutenga chumba maalum cha Wazee ili wanapofika kituoni hapo waweze kupata huduma za afya wakiwa katika hali ya utulivu.
Aidha, Mwenyekiti huyo wa Jumuia ya Wazazi Taifa amepongeza Wataalam na wasimamizi wa mradi wa maji Itete kwa hatua uliofikia mradi huo na kuongeza kuwa mradi huo ukamilikea ndani ya wakati ili wakazi wa Itete waweze kupata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ndugu Fadhili Maganya pia ametoa wito kwa Wanawake, na Vijana kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kupiga kura Oktoba 11-20 na kushiriki kwa wingi kupiga kura Novemba 27 ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kuleta maendeleo Wilayani Malinyi.
Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa Jumuia ya Wazazi Taifa amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Mhe. Sebastian Waryuba, na Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Khamis Jaaphar Katimba kuwafikia Wananchi katika maeneo yao ili kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili, kufuatilia na kusimamia kikamilifu zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye Ulemavu.
Ofisi ya Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi
Postal Address: 18 Malinyi, Morogoro
Telephone: 0643111999
Mobile:
Barua pepe za watumishi: ded@malinyidc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.